-->

Header Ads

TRENI YA DELUXE YAPATA AJALI,HAKUNA VIFO VILIVYORIPOTIWA


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa leo  Januari 29, 2017 mnamo  saa 9:40

alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka
Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa
9 yamepata ajali . Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu
yameacha njia.



Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha
mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa
hospitali kwa matibabu zaidi. 


Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha
uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika
Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame  Mbarawa 
.Mkuu wa TRL Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi , Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd
Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S.
Chillery wako  katika eneo la ajali! . 





Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya
treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es
Salaam na  inatarajiwa kuwasili saa 2
usku.





Aidha
 uongozi wa TRL umehakikisha umma na
wateja wake kuwa njia ya reli  kati ya Ruvu
na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji  zirejee kama kama kawaida. 





Imetolewa na Afisi ya
Uhusiano:


 Kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 

Ndugu Masanja Kungu
Kadogosa


Januari 29, 2017

DAR ES SALAAM 

No comments

Powered by Blogger.