-->

Header Ads

JPM: Marufuku askari kufyeka mashamba ya bangi

Rais Magufuli amepiga marufuku askari wa jeshi la polisi, na viongozi wote wa serikali wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na makatibu wakuu kujishughulisha na kazi ya uchomaji na uteketezaji wa mashamba ya bangi na badala yake ameiagiza polisi kuwatumia wanakijiji kufanya kazi hiyo.
Ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

“Kama bangi imelimwa karibu na kijiji, shika kijiji kizima, kuanzia wazee, wamama mpaka watoto ndiyo wakafyeke hilo shamba, maaskari wangu hawakuajiriwa kufyeka mashamba ya bangi. … Usiwatume maaskari wako kufyeka bangi, mwisho wataumwa nyoka mule, mmevaa sare nzuri halafu mnafyeka bangi , mnaaibisha jeshi”, - Rais Magufuli.

No comments

Powered by Blogger.