-->

Header Ads

JPM amwaga mabilioni kwa jeshi la polisi

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametoa bilioni 10 kwa jeshi la polisi ili zitumike katika ujenzi wa nyumba za kuishi askari wa vyeo vya chini.
“Mimi nimeoa kambini, mke wangu ni mtoto wa askari polisi, na baba mkwe amefariki akiwa sajenti…ninayajua maisha ya polisi…ni magumu sana.
Kwa kutaambua hilo, leo nitatoa shilingi bilioni 10 ili zikasaidie kujenga nyumba za polisi wenye vyeo vya chini,” alisema Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na Wafanyabiashara mkoani Arusha.
Nyumba hizi zimejengwa baada ya zilizokuwepo kuungua moto mwaka jana.
Rais Magufuli aliwataka askari anchi nzima kutembea kifua mbele na kasema kwambaa yeye kama Amri Jeshi Mkuu, yuko pamoja nao na hatawaacha.  “Maneno ya kashfa na kebehi mnayopewa na watu wachache yasiwakatishe tamaa. Mimi niko pamoja nayi…sita waacha,”

No comments

Powered by Blogger.