-->

Header Ads

IGP Sirro awaonya wanaohamasisha maandamano katika mitandao

Inspector General wa Pilisi nchini, (IGP) Simon Sirro waonya wale wote wanaohamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii kuacha mara moja na kusema kwamba jeshi la polisi liko macho wakati wote.
"Upo uhamasishaji kwenye mitandao, na hili niseme… mimi naamini wameshaandamana kwenye mitandao, wameshamaliza maandamano yao, la msingi sasa tujenge nchi yetu" alisema IGP Sirro wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wafanyabiashara Mkoani Arusha.
“Jeshi la polisi liko imara kweli kweli…ninawaomba wale wote wanaopanga kufanya maandamano na vurugu ili kuvunja amani ya nchi kuacha mara moja…na kama wataona ushauri huu haufai basi tusilaumiane,” alisema IGP Sirro.
Kwa upande wake, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba alisisitiza kwamba Tanzania imeendelea kupata alama za juu katika masuala ya amani hapa dunia.
“Sisi tumeshika nafasi za 50 bora duniani. Kwa Afrika Mashariki sisi ni namba moja,” alisema Waziri Nchemba
“Wapo Watanzania wanaosikiliza maelekeza ya madaktari...na wapo wale ambao wanasikiliza ramli za waganga wa kienyeji, kwa nini wanashindwa kusikiliza maelezo ya kiusalama tunayowapa?”- alisisitiza Waziri  Nchemba

No comments

Powered by Blogger.