-->

Header Ads

Jeshi la polisi ‘latimua’ askari 458

Jeshi la polisi Tanzania limesema limewafukuza kazi askari zaidi ya 458 kwa sababu za utovu wa nidhamu na kwamba utaratibu wa kuendelea kuwatoa askari wote wasio na nidhamu katika jeshi hilo bado unaendelea.
“Nidhamu katika jeshi la polisi ni jambo ambalo tunaliwekea msisitizo mkubwa sana. Tunaendelea kuimarisha nidhamu katika jeshi la polisi,” alisema IGP Sirro wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi zilizojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na Wafanyabiashara Mkoani Arusha.
Alisema kwamba kuanzia mwaka 2015 mpaka 2018, Jeshi limefukuza zaidi ya askari 458 wasio na nidhamu.
Akizungumzia juu ya hali ya usalama nchini, IGP Sirro alisema kwamba mauaji ya vikongwe na mauaji mengine yamepungua kwa asilimia 17.8 katika kipindi cha January - February, 2018 ikilinganishwa na Asilimia 9.11 katika kipindi cha mwaka 2017.
"Katika kipindi cha January - February, 2018 jumla ya matukio ya Jinai yaliyoripotiwa ni 96363 ikilinganishwa na matukio 104073 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2017" alisema IGP Sirro.

No comments

Powered by Blogger.