-->

Header Ads

Fahamu Namna ya kutibu homa ya matumbo katika kuku



Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na huwapata kuku wa umri wote. Mara nyingi ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa kuku wagonjwa kwenda kwa kuku wasio wagonjwa kupitia kwenye mayai , chakula chenye kinyesi cha kuku wenye ugonjwa pia watu iwapo watabeba vimelea na kuja navyo kwenye banda.

Jinsi unavyoambukiza:
1.    Kuku asiye mgonjwa kula vimelea vya ugonjwa kupitia kinyesi cha kuku mgonjwa kwenye chakula.
2.    Kuku mgonjwa huweza kurithisha vifaranga wake kupitia mayai yaliyotagwa.
3.    Watu na vyombo vya usafiri wanaweza kuhamisha ugonjwa kutoka sehem hadi sehemu.
4.    Vyakula vya kuku kutoka sehemu yenye ugonjwa kwenda kusiko na ugonjwa.
5.    Mizoga ya kuku yenye ugonjwa ikipelekwa sehem isiyo na ugonjwa.

Dalili za ugonjwa huu ni;
a) Homa Kali
b) Manyoya husimama
c) Kinyesi kuonekana kuganda sehem za nyuma.
d) Kukosa hamu ya kula.
f) Kuku kudhoofika.
g) Kiwango cha utagaji hushuka.

Kinga:
Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa.Kuku wagonjwa watengwe na kupewa tiba ya antibiotic.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji.

Matibabu:
Dawa aina ya Oxytetracycline(OTC)au Salfa ambayo huchanganywa kwenye maji na kupewa kuku kwa siku 5 hadi 7.

No comments

Powered by Blogger.