Watahiniwa 385,938 Kidato cha nne Wanaanza Mitihani Kesho JUMATATU

Jumla ya watahiniwa 385,938 wamesajiliwa kwa ajili ya kufanya mtihani wa
kidato cha nne mwaka huu ambapo mitihani hiyo inatarajiwa kuanza rasmi
kesho kwa nchini nzima.
Akitoa taarifa za mitihani hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani
la taifa Dk Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa 385,938,watahiniwa
wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kujitegemea ni 62,425 akaongeza
kuwa taratibu za mitihani lazima zifuatwe.
Aidha Katibu huyo amesisitiza kuwa bado kanuni na sheria za mitihani
haziruhusu watu wasiohusika na mitihani kufika katika maeneo ya shule
kwani watahiniwa wanahitaji utulivu mkubwa na hivyo jamii na watu wote
waelewe hivyo.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments