Waziri wa mifugo na Uvuvi amepiga marufuku Uuzwaji Holela wa wanyama Wanaokamatwa Kwenye Hifadhi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina amemepiga marufuku mifugo
inayokamatwa kwenye hifadhi mbalimbali nchini kupigwa mnada bila maafisa
mifugo kuipima na kujiridhisha ili kuepuka kuenea kwa magonjwa ya
wanyama hao sambamba na kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wamekuwa
wakipokea na kubeba dhamana ya mifugo kutoka nje ya nchi huku wakidai
kuwa ni ya kwao.
Akishiriki zoezi la ukamataji wa mifugo zaidi ya mia moja na sabini
iliyoingia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutoka nchi jirani ya Rwanda
Waziri Mpina amesema ni kinyume cha sheria na amewataka wafugaji
wanaokamatiwa mifugo yao kujitokeza mara moja ili kuepuka usumbufu
unaojitokeza.
Aidha Waziri Mpina amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali
wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kukubali kubeba dhamana ya mifugo
kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments