VIDEO: Askari akatwa sikio na kuuawa Dsm
Kwamujibu wa kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam SACP
Lazaro Mambosasa, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM mnamo
tarehe 21/10/2017 majira ya saa 06:O0hrs huko maeneo ya kambi ya polisi
kikosi cha kutuliza ghasia Ukonga Makao makuu mkoa wa kipolisi Ilala,
askari wakiwa kazini walikuta mwili wa marehemu X-G 475 PC CHARLES YANGA
ukiwa pembeni mwa uzio wa kambi hiyo akiwa ameanguka chini huku
pikipiki yake aliyokuwa akiendesha ikiwasha taa za tahadhari(hazards
light), mwili huo ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye paji la uso na sikio
moja likiwa limekatwa kabisa.
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu

No comments