Serikali yatenga Sh530 bilioni kwa ajili ya wafanyakazi
Dar es Salaam. Serikali imetenga Sh531 bilioni kwa ajili ya
wafanyakazi waliopandishwa madaraja ambao taarifa zao zimehakikiwa na
hazina utata.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas alisema kwa
sasa Serikali imemaliza mchakato wa awali wa kusafisha watendaji hewa
kwenye mfumo na wale ambao wataonekana kuwa ni halali mchakato wa
kupandisha madaraja utaanza.
Alisema kwa sasa Serikali
inatekeleza na kufanyia kazi agizo la kupandisha wafanyakazi madaraja na
katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha Serikali imetenga Sh487.7
bilioni kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi baada ya kuanza kwa mfumo mpya
na kuondoa wafanyakazi wenye utata.
“Mchakato wa
kupandisha madaraja unaendelea na wengine ambao hakuna mchakato mrefu
kuwapandisha madaraja wamekwishapandishwa na wamelipwa na tayari katika
robo hii Sh531 milioni zimeshalipwa kwa waliopanda katika ngazi zisizo
na utata,” alisema.
Dk Abbas alisema Serikali imetenga
Sh35.2 bilioni kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya mishahara kwa
wafanyakazi huku Sh70.4 bilioni zikilipwa kwa ajili ya madai ya
wafanyakazi sehemu kubwa ikiwa ni madai yasiyo ya mishahara kwa mwaka
2016/17 katika robo hii ya kwanza.
Awali mkurugenzi
huyo alikanusha taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kuhusu kauli ya Rais John Magufuli
kutopandisha mishahara kwa wafanyakazi na Dk Abbas alisema kauli hiyo
ililenga posho za madiwani na si wafanyakazi wote.
“Si
kweli kuwa kauli ilijikita kwa wafanyakazi wa umma bali ni madiwani
waliotaka kuongezewa posho kutoka Sh350,000 hadi 800,000 na si
wafanyakazi na sisi kama Serikali tutawachukulia hatua walioeneza
taarifa hii ya uongo,” alisema.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments