Abiria wapanda mabasi ya Udart kwa kugombea
Abiria wanaotumia mabasi yaendayo haraka ya kampuni ya Udart wamepata adha ya usafiri baada ya magari zaidi ya 20 kuharibika kutokana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Udart, mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.
Mwandishi wa Mwananchi ameshuhudia leo Jumatatu Oktoba 30,2017 asubuhi abiria wakitumia nguvu kupanda mabasi ili kuwahi kwenye shughuli zao.
SOMA ZAIDI-Abiria wa mwendokasi kama wa daladala
Waliokuwa wakihangaika zaidi ni wanafunzi wa kidato cha nne ambao wameanza mitihani yao ya Taifa leo.
Baadhi ya vituo ambavyo abiria wamekuwa wakigombea mabasi ni vya Kimara, Mbezi na Ubungo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameshaagiza watoa huduma ya mabasi hayo kuhakikisha yaliyoharibika yawe yametengenezwa ifikapo Alhamisi Novemba 2,2017 ili kuwaondolea adha abiria.
KWA HABARI ZA HIVI PUNDE TANZANIA LEO jiunge na AKISITV na www.akisitv.com updates zote utazikuta humu
No comments