Raphael Varane asaini mkataba mpya Real Madrid
Mchezaji huyo, 24, raia wa Ufaransa amecheza mechi tatu kati ya nne za mwisho za Madrid katika michuano yote baada ya kukosa mechi tatu za mwanzo wa msimu.
Varane sasa amemwaga wino kusaini mkataba ambao utambakisha Bernabeu hadi 2022.
Mfaransa huyo amejiunga na Madrid 2011 na amefanikiwa kucheza mechi 196 katika klabu hiyo kwenye michuano yote, na kufunga magoli 10.
Varane aliisadia Los Blancos kutwaa mataji matatu Ligi ya Mabingwa, pamoja na taji moja la La liga.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments