"Raphael Daud atatupa ubingwa msimu huu" - Ibrahim Ajibu
Ajibu ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwa wapinzani wao wakubwa, Simba, amefanikiwa kufunga magoli mawili katika michezo 4 ya Ligi Kuu hadi sasa.

Ajibu amesema ana vutiwa na kiungo huyo wa zamani wa Mbeya City, Daud kuwa amekuwa akionyesha uwezo wa juu katika kila mchezo wao jambo ambalo limekuwa likimfurahisha yeye na kumpa imani kuwa kiungo huyo ataibeba timu hiyo na kuipa ushindi kwenye kila mechi, aliongee hivyo wakati akihojiwa na gazeti la michezo la Champion.
"Kwangu nimekuwa nikikoshwa na kiwango cha kiungo wetu, Raphael Daud, katika kila mchezo wetu na hata kwenye mechi iliyopita mbele ya Ndanda FC, alionyesha uwezo mkubwa na wa hali ya juu, nadhani kwa kupitia uwezo wake itakuwa rahisi sana kwetu kushinda kwenye kila mchezo na pia tunaweza kutwaa ubingwa kama atadumu muda mrefu bila kuumia,” alisema Ajibu ambaye mpaka sasa ameshafunga mabao mawili.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments