KISIWA CHA ZUNIGA (2)
Na Adalgisa kweka
Alijikunyata binti yule akisubiria kuinuliwa juu kwani tiyari alishaitwa.
"WEWEE!" sauti ile ilisikika Tena, mara hii kwa ukali zaidi nakumfanya kijana yule afanye kitubio cha fastafasta kabla uhai wake haujachukuliwa na kiongozi Huyo.
"MZAWA Kuna tatizo gani?" ilikuwa ni sauti iliyotokea mwisho kabisa wa chumba hicho sauti hiyo ilikuwa tumaini jipya kwa kijana yule wa kike ijapokuwa Jina alilotumia kumuita kiongozi Huyo lilikuwa ni gumzo katika masikio ya msikiaji.
"Kuna kijana mmoja nahisi kashuhudia siri ya kisiwa afu kakimbia ndo namtafuta nliona kivuli cha mtu kimeketi pale nkajua ndo yeye kumbe ni wewe MZAWA mwenzangu"
"oooh" alimsogolea karibu MZAWA mwenzie ili kumnong'oneza "mimi nko doria kwenye hiki chumba MZAWA mkuu alinipangia siunajua vijana Hawa hawajagaiwa kimakundi bado usihofu atapatikana tu Huyo kijana"
"Sawa MZAWA" MZAWA aliondoka.lakini kumbe walichonong'onezana wakijua ni siri kumbe kijana Huyo wanayemuwinda aliyasikia mazungumzo Yao yote.ijapokuwa moyo wake ulitulia bado alibaki na vitendawili ambavyo vijana wenzie hawakuweza mtegulia labda wazawa tu.alitamani angempata mwenziye ambaye aliyasikia mazungumzo ya wale wazawa wawili aku kuyaona yaliyokuwa yanajiri nje ila hakujua kama yupo aluchojua yeye ni kwamba alishuhudia vitu asivyotakiwa shuhudia na alitakiwa akae kimya kama hataki baya lolote kumkuta. Kijana yule hakuweza lala mbaka aliposikia sauti ya MZAWA iliyokuja kuwaamsha naye akaamka na wenzie. Aliamuka nakuangalia pale kitandani vizuri kama haja yake ndogo ilililowesha godoro lake Sana nakama ulishuka mbaka Chini.kwa bahati nzuri haja yake ndogo haikuleta maafa isipokuwa Hali ya yeye kukosa nguo ya kuvaa Hilo lilimtatiza Sanaa,hakuzoena na mtu yeyote yule zaidi ya yeye mwenyewe hapa ndipo alipokumbuka kauli ya mama yake ambaye tangu aingie hapo Jana hakupata nafasi hata kidogo yakumuwaza. "Tuli mwanangu, Kuna siku sitokuepo inabidi ujifunze jinsi ya kujenga mahusiano na watu ili kwenye shida upate kusaidiwa." yalikuwa ni maneno mazito ya mama yake Tuli yaliyopita kama maandishi ya matangazo kwenye Televisheni.maneno Yale yalimpa nguvu yakutazama upande wake WA pili ambapo alikutana na sura ya mviringo iliyopambwa kwa mkato wa tamaa ikimuangalia yeye.alikuwa ni binti wa kiislamu kutokana na mavazi aliyovaa yakuufunika mwili wake wote,akiwa anamuangalia kijana mwenzie alimsikia akimwambia.
"Chukua hii via"ilikuwa ni sauti ya yule binti wa kiislamu. Tuli aliangalia mkononi mwake aliiona kuwa alikuwa amempa nguo yakujistili ni kama alikuwa anazisikia fikra za Tuli mbaka akaamua kumsaidia.
"Asante Sanaa"Alishukuru kwani huo ulikuwa Masada mkubwa kwake kwa wakati huo.aliichukua papohapo nakuanza kuivaa ilikuwa ni zile skin-tight ndefu za kisasa almaarufu kama leggings ambazo watu hususani waislamu wengi sikuhizi hupenda kuvalia ndani ya Dela.
"naitwa sailat" yule kijana mwenzie alijitambulisha huku sauti yake ikiwa na lafudhi ya kipemba kwa mbali.
"mini naitwa Tuli nashukuru kukufahamu" alimtabasamulia ishara ya kuridhika kuwa hatimaye alimpata ndugu na rafiki mmoja kisiwani Zuniga.
"Pole kwa yaliyokukuta "
"Asante"aliitikia ingawa hakujua pole hiyo ilikuwa ya nini hasa kwani alishapitia majanga mawili Tiyari. Fikrani kwake alihisi labda sailat alishuhudia yote Yale labda ndiye aliyemziba macho Lakini hakujua angeazaje uliza alihofia pia huyu anaweza kuwa mzawa naye kwani kitendo chakutokufunua Shuka Lake usoni usiku ilikumuona mzawa aliyeitika kauli ya kiongozi yule mshurutishi ambaye naye alikuwa mzawa kilimuuma Sana kwani laiti angemuona anafananaje asingeweza kuwa na Chembechembe za hisia kuwa saluat ni mzawa.alipomaliza kuvaa aliweka kitanda vizuri huku saluat akimsaidia Kisha wakaondoka kuelekea wanapohitajika. Wakiwa njiani waliendelea na mongezi Yao.
"wewe ni mwenyeji wa wapi?" aliuliza saluat.
"Mwanza ila nimezaliwa nakukulia dar-es-salaam"
"aah mimi shinyanga"
"Duu umefikaje sasa huku?"lilikuwa ni swali laajabu kuuliza kwani jibu lilijulikana lakini bado aliliuliza,alihisi labda atakuepo mtu au watu watakao kuwa wanajua angalau kitu chochote.
"sitakagi kuikumbuka hiyo siku ingawa nimeshindwa kuifuta kichwani mwangu, watu walikuja ambao hata hatuwafahamu, hawakusalimia wala kuketi angalau tuwape maji wanywe walinichukua kwa nguvu mbele ya wazazi wangu.mama na baba walipambana lakini waliambulia vipigo vya mbwa mwitu na damu kuwatoka bado hawakuweza niokoa kwani watu wale walinichukua nakuniweka ndani ya Gari Yao kama mzigo ambapo nilikutana na vijana wengine wote tukiwa na vilio visivyopimika na kama haitoshi walitufunga vitambaa usoni hakuna tulichokiona zaidi ya kusikia tu Tena kusikia kwenye hatukusikia kitu chochote zaidi ya mngurumo wa Gari Lao la kisasa lililokuwa refu mithili ya Costa."
"duuu pole Sana" maelezo yake hayakutofautiana na ya kwake isipokuwa yeye katika harakati za wazazi wake kumpigania kwa nguvu mmoja alipigwa risasi ambaye ni baba yake hakujua kama yuko Hai au amekufa na je kama yuko Hai anaendeleaje.mawazo haya yalimfanya machozi yamtokee, Saluat alimuonea huruma ndugu yake huyo mpya alimsogelea nakumbembeleza.
"Yana mwisho haya"alimpa moyo ingawa ni ukweli usiopingika kuwa hakukuwa na mtu yeyote aliyejua mwisho wake.
"Nina maswali mengi najiuliza sipati Majibu. Hiki kisiwa kiko sehemu gani hasa?je Raisi anajua au wanatutafuta yaani hata kwenye habari tunatangazwa kweli kuonyesha kuwa nguvu kazi yataifa imepotea na je yule mheshimiwa-"
"nafikiri tuishie ha-po"Saluat alimkatisha tuli mazungumzo kwani mmoja wawazawa alikuwa amefika eneo walilosimama.
"Nyie vijana wakike mnafanya nini hapa?"ilikuwa sauti ya mzawa iliyosheheni ukali. Sauti zao zilifanana kama vilio vya vifaranga wakuku.
"a-m-aaa rafiki ya-ngu alikuwa ana-ji-sikia vi-ba-ya.."aliongea kwa hofu Sana maana hakujua ni neno gani lingetoka mdomoni kwa mtawa huyo
"HATUNA RAFIKI KISIWANI!!"ilitoka sauti ambayo kama mtu aliyesimama naye anapresha angezima papohapo kwani ilishtua Sana na ilikuwa ya ukali
"Sawa a-fa-nde"aliongea kwa kusita Sana
"HATUNA AFANDE KISIWANI Kijana!! Sisi ni wazawa wa Hiki kisiwa,Leo watawajuza vizuri" akiwa anaongea wao walimchunguza mzawa huyo ndipo walipoona nembo ndogo imebandika kwenye shati Lake ikiwa na picha kama ya mlima huku ikiwa na maneno yaliyosomeka MZAWA LUGAS SK.kwa saluat ilikuwa Mara ya kwanza kuona na kusikia neno mzawa Lakini Hali ilikuwa tofauti kwa Tuli kwani yeye alikuwa akipigia mstari majibu yake.
"HAYA HARAKISHENI MUENDE KWENYE MKUTANO". Dakika sifuri waikuwa wameshafika kwenye mkutano ambapo walimkuta mmama anaongea.
"Vijanaa!Leo tutawagawa kimakundi ilikukamirisha zoezi hili mmeona vile vyumba(alinyoosha kidole chake kuelekea Jengo la ukubwa kiasi likiwa na vyumba vingi vilivyokuwa na namba kwa ujumla vilikuwa vyumba ishirini.)wote mmeviona basi mtapanga foleni katika kila chumba mtaingia ndani mtakutana na wazawa yeye atawapa maelekezo zaidi.kabla sijasahau Hawa viongozi mnaowaona wanaitwa wazawa majina Yao yamebandikwa kwenye nguo zenu,pale mtakapo toka kwenye hiko chumba mtakuwa wenyeji tiyari SHERIA ZA KISIWA ZIFUATE UKIKIUKA ADHABU YAKE NI KIFO!!" alimaliza mikutano ya kisiwa haikuwa yakawaida haimalizi na shukrani wala Asante.Kauli ya mwisho ya yule mama ambaye katika mtazamo WA haraka hakupendeza kuitwa mama ilimrudisha Tuli nyuma katika tukio alilolishuhudia Jana usiku ghafla alianza kutetemeka.
"nini tatizo Tuli"aliuliza saluat baada yakuona mabadiliko yake ghafla ila si saluat tu aliyeona Bali na vijana wengine waliokuwa karibu.
"hapana nahisi Homa sij-ui"aliuficha ukweli hakuhitaji mtu ajue kwani kungefanya ajulikane.
"sijui tunafanyeje sa-"
"usihofu itaisha ntajikaza" alidanganya hakutaka saluat akaongee na mzawa yeyote.yule mama aliondoka na wao wakaanza kujipanga katika mistari katika vyumba hvyo ilikugawa kimakundi. Katika mkutano huo Hawa kuwaona wale vijana wenzao ambao ni wenyeji,zaidi yakupishana nao barabarani wakiwa kwenye kasi mithili ya roketi.
Saluat na Tuli walipanga mstari katika chumba namba 5 wakisubiria zamu Yao ifike huku kimya kikitawala. Wakiwa kwenye mstari wamesimama Tuli alishtushwa na ujio WA kijana wa kiume pembeni yake ambaye hakuwa kwenye mstari akiwa anamshngaa kwa mshtuko yule kijana alimuongelesha.
"unamfahamu yule aliyekuziba macho" maneno Yale yalimshtua zaidi kiasi chakumfanya apatwe na wasiwasi juu ya kijana huyo.
"nilishuhudia kilichoendelea pale nje,yule jamaa-" kabla hajamalizia alichosema Tuli alimziba mdomo nakusogea Kisha kumuachia sehemu asimame mbele yake.hakutaka kijana yule aendelee kuongea chochote kuhusiana na kisiwa hiko.aliutoa mkono wake kwenye mdomo WA yule kijana lakini kama wasemavyo sikio la kufa halisikii dawa ndivyo ilivyokuwa kwa yule kijana kwani Tuli alipoutoa mkono wake kwenye mdomo wake aliendelea kubwabwaja tena, raundi hii aliongea mambo yaliyowashtua vijana wengine waliokuwa karibu Yao.
"nahitaji kujua kama unamfahamu yule jamaa dada yangu, yule atatusaidi kutoroka".Saluat alikuwa haelewii ni nini alichomaanisha yule kijana huku Tuli akihisi moyo wake umepigwa ganzi kubwa huku akimshangaa kijana huyo waajabu ambaye hakuelewa madhara ya maneno aliyoyasema endapo yatasikika na wazawa.
"sshhshhh kaka usitutafutie kifo" saluat alimwambia yule kijana WA kiume ijapokuwa hakuelewa kilichoendelea lakini maneno ya mwisho ya kijana yule hayakuwa mazuri kuropokwa hadharani.hata hivyo onyo la saluat halikusaidia kwani wakiwa wamesimama walimsikia mmoja wa kijana aliyekuwa mbele ya yule kijana mropokaji akiita kwa nguvu
"WAZAWAA!! NJOO KAMATA WASALITI HAWA" sauti Yake ilifanana na wazawa ilisheheni uzito na hasira. Kama haitoshi aligeuka nyuma nakutoa kinembo kilichokuwa kwenye mfuko wa shati Lake nakukibandika kwenye shati Lake ndipo Jina liliposomeka MZAWA ZIKU DK. Tuli aliimshika mkono saluat alihisi damu imemuishia mwilini. Yule kijana aliweka mkono wake kwenye bega la kushoto kwa MZAWA yule Kisha alifungua kinywa chake kilichokuwa kizito huku macho Yake Yakiwa mazito aliuliza swali kinyonge.
"Wewe ni MZAWA?".....ITAENDELEAA..

No comments