BREAKING NEWS: TUNDU LISSU APIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA DODOMA
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.abari zilizotufikia hivi punde ni kwamba RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA NCHINI TUNDU LISSU AMEPIGWA RISASI na watu wasiojulikana akiwa Dodoma Leo.. Taarifa zinataarifu kuwa tayari Tundu Lissu amewahishwa Hospital ya mkoa ya Dodoma.
Mwenyekiti wa Chadema taifa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo..
Kwa taarifa zaidi endelea kuwa nasi

No comments