USISHANGAE YANGA IKIWATAMBULISHA HIMID MAO NA NGASSA JUMAMOSI HII.. TAARIFA KAMILI HII HAPA
BAADA ya Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga kumalizana na kiungo wa
Mbeya City, Rafael Daud, uongozi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara umepanga
kufanya jambo kubwa katika usajili wiki hii.
Mmoja wa wachezaji ambao wanatajwa kuwa watasajiliwa na klabu hiyo wiki
hii ni Himid Mao wa Azam FC, kwani Yanga wana mpango wa kufanya mazungumzo na
uongozi wa Azam ili waweze kufikia mwafaka na kumsajili.
Taarifa ambazo BINGWA limepata zinadai kuwa, Kocha Mzambia, George
Lwandamina, juzi alikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika,
na kuzungumza naye masuala ya usajili, ikiwamo kusisitiza usajili wa Mao.
Chanzo hicho kimedai kuwa, Yanga wakimalizana na Azam, Mao ataonekana
uwanjani rasmi Agosti 5, mwaka huu, timu hiyo itakapomenyana na Singida United
katika mchezo wa kirafiki, ambao winga wake wa zamani, Mrisho Ngassa, pia
anatajwa atakuwapo.
BINGWA lilipomtafuta Nyika kuzungumzia mchakato wa usajili unaoendelea, alisema
wanatarajia kuongeza wachezaji wawili, ambao ndio watafunga zoezi hilo msimu
huu.
Alisema mchezaji mmoja itasajiliwa katikati ya wiki na mwingine ni
mwishoni mwa wiki, ambapo washamsainisha uwanjani baada ya mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya Singida United.
“Siwezi kuweka wazi kuwa ni wachezaji gani tunaowasajili, hiyo ni ‘surprise’,
hivyo subiria siku hiyo utajua akina nani,” alisema Nyika.
Kuhusiana na usajili wa Mao, Nyika alisema mchezaji huyo si mbaya, kwani
wakimpata atawasaidia kwenye timu yao.
“Mfano wewe ungekuwa kocha ungemkataa kweli mchezaji kama Himid? Hivyo
kama kocha atatuambia anamuhitaji tutamsainisha,” alisema Nyika.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Azam, Idrissa Nassor ‘Father’, alisema mpaka
sasa hakuna timu iliyokwenda kwao ikihitaji kufanya mazungumzo yanayomhusu
kiungo wao, Mao.
Alisema Mao bado ni mchezaji wao halali na juzi alijiunga na wenzake kwa
ajili ya mazoezi yanayoendelea katika Uwanja wa Azam Complex, kujiandaa na Ligi
Kuu msimu ujao.
“Si Yanga wala timu yoyote kutoka nje iliyokuja kwetu kutaka kufanya
mazungumzo ya kumsajili Mao,” alisema Father.
source;
BINGWA
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments