WHO watoa tahadhari dhidi ya ugonjwa Wa kisonono
Shirika la afya Duniani WHO limetoa tahadhari kuhusiana na ugonjwa wa zinaa wa kisonono na kusema kuwa tiba dhidi ya ugonjwa huo imeanza kuwa sugu kutokana na dawa zake kushindwa kukabiliana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni katika mataifa 77 tofauti Duniani,
WHO imebaini kuwa maambukizi ya ugonjwa huo katika nchi za Japan, Ufaransa na hispania hayatibiki kabisa.
Pia shirikika hilo limeongeza na kusema wengi wa wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi masikini ambazo zinavifaa duni kudhibiti ugonjwa huo.
Ni vyema kutumia kondom ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huu Wa kisonono.




No comments