-->

Header Ads

WATANZANIA WALIPA KODI WAFIKISHA TRILION 14.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017





Mamlaka ya mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh trilioni 14.4 kwa mwaka wa fedha 2016l17

Baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2016/17 hapo juni 30, mamlaka ya Mapato TRA imetoa taarifa za makusanyo hayo kupitia Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi RICHARD KAYOMBO, katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam 

Mamlaka hiyo imekiri kuongezeka kwa makusanyo hayo, kwa asilimia 7.67 kulinganisha na mwaka wa fedha uliopita ambako katika mwezi juni ilikusanya jumla ya trilion 1.37.

Pamoja na hayo T.R.A inawashukuru wananchi wote walipa kodi kwakuwa inawezesha serikali kuchukua majukumu yake.

Pia mkurugenzi wa huyo amewakumbusha wananchi kuzingatia ulipaji wa kodi za majengo ambao muda maalumu uliotelea umesalia siku nne tu kufikia kikomo hapo tarehe 15 julai.

Watu wasio penda kudai au kutoa  risiti kupitia mfumo wa utoaji risiti za EFD  wahimizwa ,'' inawezekana mmeona maeneo mbalimbali katika biashara mbalimbali tumebandika stika zinamuonesha mtu anayenunua bidhaa kuwa mahali hapa kuna mashine za EFD  kwahiyo anayenunua bidhaa asitoke bila kudai risiti.'' Mkurugenzi Kayombo.

Aidha TRA  inawatahadharisha watu wote wanaotumia njia za udanganyifu katika utoaji wa risiti hizo, endapo watabaininika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 ''usiishie tu kudai risiti,bali dai risiti lakini nenda mbali zaidi ikague kama ni tarehe sahihi ya leo ama angalia kiasi kilicholipwa kama kipo sawa, kwasababu kuna mtindo umezuka kwamba watu wanakupa risiti kwasbabau umedai risiti lakini wanakupa ya juzi ama kiwango ulicholipa si kilichopo kwenye risiti, tumetambua hilo na tunachukua hatua zinazostahili" alisisitiza Mkurugenzi Kayombo.



No comments

Powered by Blogger.