-->

Header Ads

WAJUE WAIGIZAJI WATANO MATAJIRI DUNIANI.

Hii ndiyo orodha ya waigizaji wakiume watano matajiri duniani  ya mwaka huu wa 2017.

1)Jerry Seinfeld

Jerry ni muigizaji ,mchekeshaji,mtunzi na muongozaji wa filamu,alizaliwa Brooklyn,New york  huko nchini marekani mwaka 1954.Jarida  ya Forbes limemtaja Jerry  Seinfeld kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 820.Baadhi ya filamu zake ni Diary of a mad black woman,a familly that pervs.

2)Shah Rukh Khan

Ni muigizaji kutoka nchini India ambaye mashabiki wanapenda kumuita King Khan ambaye anasemwa kuwa amecheza zaidi ya filamu 75 za kihindi.Khan anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 620.Baadhi ya filamu za Khan ni My name is Khan ,The Don,Koyla na nyingne nyingi.

3)Tyler Perry.

Ni muigizaji na mtunzi kutoka huko nchini Marekani aliyezaliwa mwaka 1969 huko New Orleans,Marekani.Tyler anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 600 na kumuweka kuwa muigizaji wa tatu kwa utajiri mkubwa duniani.

4)Tom Cruise

Anajulikana sana kwa filamu zake maarufu za Mission Impossible ambazo zimempa umaarufu mkubwa na kumpa tunzo nyingi.Tom Cruise ametajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 480.Baadhi ya filamu nyingine zilizompa umaarufu na mafanikio makubwa ni pamoja na Top gun,Rain Man ,Tropic Thunder.

5)Amitabh Bachchan

Ndio muigizaji mwenye heshima nchini India ,anajulikana kama baba ya Bollywood ambaye amedumu kwenye tasnia ya filamu kwa miongo mitano.Amitabh anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani 420 akiwa muigizaji watano kwa utajiri duniani.Baadhi ya filamu zilompa umaarufu Amitabh ni Sholay,paa,Dewaar na nyingine nyingi.

No comments

Powered by Blogger.