-->

Header Ads

Viongozi hasimu wa Libya wakutana Paris, wakubali kusitisha vita

Kamanda wa majeshi ya Libya mashariki mwa nchi hiyo, Jenerali Khalifa Haftar na Fayez al Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo, magharibi mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika wamekubaliana kusitisha vita kwa masharti.
Haya yanajiri baada ya wawili hao kukutana katika mazungumzo ya moja kwa moja, yaliyosimamiwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron katika eneo la La Celle Saint-Cloud, nje kidogo ya mji mkuu Paris jana Jumanne.
Katika tangazo la pamoja lililotolewa na Ofisi ya Rais wa Ufaransa baada ya mazungumzo hayo, Sarraj na Jenerali Haftar wamekubaliana kusitisha vita sambamba na kuanzisha mchakato wa kufanyika uchaguzi.
Hata hivyo tangazo hilo halijatoa maelezo na ufafanuzi kuhusu masharti waliyoyatoa viongozi hao hasimu wa Libya.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Mazungumzo hayo ya Paris ni ya kwanza ya moja kwa moja kati ya viongozi hao wawili hasimu wa Libya, tangu walipokutana katika mazungumzo ya Abu Dhabi mwezi Mei.
Libya imegawanyika katika sehemu mbili za mashariki na magharibi. Nchi hiyo ya Kiarabu ilitumbukia katika machafuko ya kisiasa na hali ya mchafukoge baada ya kupinduliwa dikteta wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011 na kufuatia uingiliaji wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na za eneo.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.