-->

Header Ads

URAFIKI WA AMBER ROSE NA BLAC CHYNA MASHAKANI.

Mastaa Amber Rose na Blac Chyna ambao ni marafiki wa muda mrefu kwa sasa hawana tena ukaribu na urafiki kama walio nao zamani.

Marafiki wa Amber Rose waliuambia mtandao wa Hollywood Life kuwa Amber Rose hakupendezwa na jinsi rafiki yake Blac Chyna alivyokuwa anaishi na mpenzi wake wa zamani Rob Kardashian.Marafiki hao wa Amber ambao hawakutaka kutajwa walisema Chyna alikua anampa shida sana Rob na ndio maana Amber alikua hapendezwi na vitendo vya rafiki yake huyo.

Suala hilo limepelekea Amber Rose kutoongea chochote kwenye tukio ambalo Rob Kardashian ambae kwa sasa wamekwisha achana na Blac Chyna kuweka picha za utupu za Black Chyna Kwenye Ukurasa wake wa Instagram wiki kadhaa zilizopita.

No comments

Powered by Blogger.