SIMULIZI MPYA YA KUSISIMUA IITWAYO ''UKURASA MPYA'' SEHEMU YA KWANZA HII HAPA
SEHEMU YA KWANZA
''..Si
kitu rahisi sana kwa mtu kama mimi Daniel, tena mwandishi maarufu niliye bobea
na kutambulika na watu wengi sana hapa nchini na hadi nje..!''
Haya yalikuwa maneno ya Daniel ambayo alikuwa
anajisemea kila kona aliyopita,
Watu wengi walipenda kumsalimia kila apitapo
lakini hakuwa anawaitikia ingawa hali hiyo haikuwa kawaida yake kabisa.
Watu wengine walisema labda kuna kitu anawaza au kuna
jambo lina mchagiza ingawa wengine pia walikuwa wanaimani huenda kuna kitu
kikubwa anaandaa, hivyo walijipa moyo na kukaa mkao wa kula kusubiri ujio
mpya wa Daniel.
Moja ya mdau wake mkubwa aliyetambulika kwa jina la
Baraka alijisemea, ‘‘sisi ni wadau wake wa nguvu sana hawezi kutukaushia kama hivi kwakuwa hata yeye anatambua jinsi gani tunavyopenda kazi zake kwahiyo bado
najipa moyo kuwa anaandaa kitu kabambe kwani huwa hakosei asee..’’
Daniel alionekana kuchanganyikiwa na kitu maana
hakuwa na furaha kabisa na alirudi mapema sana toka kazini ambavyo sio kawaida
yake kabisa.
Kila mtu aliyekutana naye alitamani kujua nini hasa kinamsibu
mwandishi huyo mwenye jina kubwa nchini.
Daniel alikuwa akiishi kwenye nyumba kubwa ya
kifahari aliyopewa na kampuni aliyokuwa akifanyia kazi na siku hiyo alienda
moja kwa moja hadi kwenye jumbna hilo hasiweze hata kuongea neno na watu
aliokutana nao njiani.
Mbali na juhudi zake za kazi amabazo zinamfanya kuingiza
kipato kizuri, Daniel alikuwa kijana mtanashati,mcheshi na mkarimu sana, mara
nyingi alipenda sana kuweasaidia watu wenye kuhitaji,na mda mwngine akiwa nje ya
kazi hupenda sana kutaniana na wadau wake ama rafiki na ndugu wanaomzunguka.
Lakini ilikuwa tofauti sana kwa siku hiyo ambapo
Daniel alipoingia ndani kwake kwenye hilo jumba la kifahari hakutoka tena.
Ni
jambo lililowashangaza wengi sana hata wale jirani zake na hata kuwapelekea kupata shauku ya kutaka
kujua nini kimemkuta Daniel siku hiyo na ikawa hivyo mpaka jua lilipo chwea
hakuweza kuonekana tena.
INAENDELEA...........
TOA MAONI YAKO.

No comments