Uholanzi yafunga bomba lake la mafuta Nigeria kwa hofu ya uharibifu wa waasi
Shirila la mafuta la Uholanzi na Uingereza la
Royal Dutch Shell, limefunga bomba muhimu la mafuta kusini mwa Nigeria
kutokana na ongezeko la vitendo vya uharibifu vinavyofanywa na makundi
ya waasi eneo hilo.
Taarifa iliyotolewa na nchini
Nigeria ambalo ni tawi la shirika kubwa la Royal Dutch Shell barani
Afrika limetangaza kuwa, kutokana na sababu za hujuma za waasi kukiwemo
kuripuliwa bomba hilo la kusafirishia mafuta, limeamua kufunga bomba
hilo kwa sasa.
Makundi ya waasi kama vile kundi la
wanamgambo linalojiita Walipizaji Kisasi wa Niger Delta la kusini mwa
nchi hiyo ambalo linaitaka serikali kugawa utajiri unaotokana na mafuta
kwa uadilifu limekuwa likihusika na mashambulizi kadhaa dhidi ya
mabomba ya kusafirishia mafuta katika maeneo tofauti ya Nigeria.
Kuzorota usalama katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya magharibi mwa
Afrika, kumeyafanya baadhi ya mashirika ya mafuta kusimamisha shughuli
zao nchini humo. Mwaka 1993 shirila la mafuta la Royal Dutch Shell,
lililazimika kusimamisha shughuli za uzalishaji mafuta katika moja ya
maeneo ya kusini mwa Nigeria.
Katika hatua nyingine watu 20
wameripotiwa kuuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi
yaliyofanywa na magaidi wawili wa kiume na kike katika kambi ya
wakimbizi karibu na mji wa kaskazini wa Maiduguri nchini humo. Habari
zaidi zinasema kuwa, katika hujuma hiyo watu watatu wameuawa na wengine
17 kujeruhiwa. Hii ni katika hali ambayo Jumatatu iliyopita pia watu
wanane waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika miripuko ya mabomu
iliyofanywa na wanawake kadhaa katika kambi hiyo ya wakimbizi.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,