VIDEO: TAIFA STARS YAICHAPA AFRIKA KUSINI, YATINGA NUSU FAINALI COSAFA.. KUKIPIGA NA TIMU HII..
Timu ya taifa Tanzania "Taifa Stars" leo imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA baada ya kuitupa nje Afrika Kusini kwa gori moja sifuri.
Mechi hiyo iliyopigwa majira ya saa 12 ya Tanzania ambapo Stars waliweza kuibuka kwa ushindi wa goli moja kwa sufuri lililowekwa nyavuni na mshambuliaji Elias Maguli.
Vile vile Maguli alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo huku kipa Aishi Manula alifanya kazi ya ziada kuiokoa Stars ambao walikuwa wanashambuliwa.
Sasa Stars itakutana na Zambia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

No comments