-->

Header Ads

MH.SAMIA SULUHU HASSAN AWATAJA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO MAKUBWA NCHINI



Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataja Bibi Titi Mohammed, Thabita Siwale, Getrude Mongela, Amina Salum Ally na Dakt. Asha-Rose Migiro kuwa ni wanawake wenye mafanikio makubwa kuanzia ngazi za familia, Taifa hadi Kimataifa tangu kipindi cha baada ya uhuru.
Mh. Suluhu aliyasema hayo leo kwenye hafla ya kukabidhiwa fimbo ya kuwa mlezi wa Tanzania Girl Guides Association(TGGA) iliyofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha Mh. Suluhu amemuunga mkono Mama Salma Kikwete, mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Dakt. Jakaya  Mrisho Kikwete kuwa wanawake wanatakiwa kuchagua watu wenye mafanikio na kuwafanya kama mfano wa kuigwa.
‘‘Kwa jinsi ninavyowaona mliopa hapa leo sina shaka kabisa kwamba uwezo huo mnao kama ilivyo kwa wenzenu mnao wawakilisha leo hapa na kama Mheshimiwa Mama Salma Kikwete alivyosema katika hotuba yake kwamba muwe tayari kuchagua wanawake wenye mafanikio ili wawe ‘role models’ wenu katika kuzifikia ndoto za kuwa na maisha mazuri’ alisema Mh.Samia Suluhu.
Pia alisistiza  na kuwatia moyo wanawake wote waliojiunga na chama hiko kuwa endapo watayafata na kuyaishi kwa vitendo mafunzo yanayotolewa ndani ya chama hiko  watafikia hatua kubwa walizofika wanawake hao.
Katika hafla hiyo Mh.Mama Salma Kikwete alikabidhi kifimbo cha malezi ya chama hicho(TGGA) kwa Makamu wa Rais baada ya yeye kuwa mlezi kwa kipindi cha  miaka 12.
Hatimaye Mh. Samia Suluhu aliwasihi wananchi kuiunga mkono Serikali kwa juhudi zinazoendelea kufanyika katika kuhakikisha Taifa linajengeka kwa misingi ya uadilifu.
‘‘Hivyo ninawasihi wananchi kuiunga mkono Serikali hasa pale tunapochukua hatua dhidi ya wahusika wa vitendo vinavyokiuka maadili yetu ya kitanzania ukiwamo uadilifu’’Alisisitiza Makamu wa Rais .
 

No comments

Powered by Blogger.