-->

Header Ads

KUHUSU MAJI MACHAFU YA MTO MSIMBAZI SERIKALI IMECHUKUA MAAMUZI HAYA..



Serikali imechukua sampuli ya maji ya Mto Msimbazi kwa ajili ya kuyachunguza ili kubaini kiwango cha sumu na ubora wa maji yake kwa matumizi ya binadamu.

Akitoa matokeo ya awali kwa wanahabari, Meneja wa  Maabara ya Mazingira  wa Ofisi ya Mkemia Mkuu, Emanuel Gwae, amesema kipimo cha maji ya Mto Msimbazi, katika eneo la Jangwani, kinaonyesha maji hayo yana kiwango cha oksijeni cha  milimita3.3.

Amesema kiwango hicho ni  kidogo na kwamba kinachohitajika ni kuanzia milimita sita.

“Hii inaonyesha namna ambavyo maji haya yamechafuka na viumbe hai waliomo humu hawawezi kuishi,” amesema Gwae.

Mchakato wa upimaji wa maji hayo umefanyika leo, Jumanne, Julai 11 katika tukio ambalo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alilishuhudia.

Katika hatua nyingine, Ofisi ya Mkemia Mkuu ilichukua sampuli hiyo ya maji ambapo Waziri Mpina alishiriki kuchota maji hayo kwa ajili ya kupimwa.

Mbali na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wadau wengine waliokuwamo ni pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bonde la Wami-Ruvu na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC).



credit:MWANANCHI


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.