JUSTIN BIERBER AKUMBANA TENA NA POLISI
Usiku wa tarehe 16 mwezi huu wa 7 msanii asiye ishiwa na mikasa Justin Bierber alisimamishwa na polisi huko Belverly Hills nchini Marekani kwa kitendo chake cha kuendesha gari huku akiwa anatumia simu.
Maofisa wa usalama barabarani waliomkamata Bierber wamesema Justin Bierber hakuwa mbishi kwani alivyosimamishwa alikubali kosa pia alitoa ushirikiano na alikubali kulipa faini.
Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kukumbwa na mkasa barabarani kwani mwaka 2014 huko mjini Miami Justin Bierber alikutwa anaendesha gari huku akiwa amelewa na aliwatolea maneno machafu polisi waliomkamata kitendo ambacho kilimfanya Bierber kufungiwa leseni yake ya udereva huku akitakiwa kulipa faini.