IMEVUJA KUHUSU MAPACHA WA BEYONCE NA JAY Z.

Je? Umeshayajua majina ya watoto mapacha wa Beyonce na Jay Z? Basi tayari habari zimeshaanza kuvuja.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umesema majina waliyopewa watoto hao ni Rumi Carter na Sir Carter. Hata hivyo hakuna kati ya Queen Bey wala Jay Z aliyethibitisha taarifa hizo.
Mapacha hao ambao mmoja ni wakiume na mwingine wakike walizaliwa wakiwa njiti June 12 ya mwaka huu na walibakia hospitalini chini ya uangalizi maalumu mpaka waliporuhusiwa siku chache zilizopita.
No comments