TAMBWE AMWAGA WINO JANGWANI HUKU DONARD NGOMA AKISAINI SOUTH..
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Burundi Amisi Tambwe amekamilisha dili la kuendelea kuitumikia klabu yake ya Yanga baada ya kuingia mkataba mwingine kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Tambwe alisaini mkataba huo juzi baada ya kurejea kutoka mapumzikoni nchini kwao Burundi hivyo kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani kwa kipindi cha miaka miwili mingine.
Wakati dili la Tambwe likiwa lishakamilika, mshambuliaji Donard Ngoma amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu ya Palokwane City ya South Afrika na kufuta tetesi za kusaini Simba au Yanga ambao walionesha nia ya kumbakiza klabuni hapo.
No comments