-->

Header Ads

SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU YA KUUZA CHAKULA NJE YA NCHI



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza rasmi kupiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya nchi.

Marufuku hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye amesisitiza kwamba, ni marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi hiyo bila kibali na kuwataka wafanyabiashara kuuza chakula kwenye maeneo yenye uhaba wa chakula nchini humo

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana wakati akihutubia Baraza la Eid al-Fitr katika  Masjid Riadha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kueleza kuwa, kuna maeneo ambayo wananchi hawakupata chakula vizuri kutokana na uhaba wa mvua hivyo wafanyabiashara wapeleke chakula kwenye maeneo hayo.

Waziri Mkuu Majaliwa ameonya kuwa kwa wale watakao kamatwa wakisafirisha mahindi nje ya nchi kinyume na utaratibu, mahindi hayo yatataifishwa na kupelekwa kwenye ghala la Taifa na magari yatapelekwa polisi.


Amesema, Serikali imepokea barua za maombi ya kupeleka chakula nchi jirani, lakini bado haijatoa ruhusa.

Akitoa tahadhari kuhusu uuzwaji wa chakula nje ya nchi, Waziri Mkuu wa Tanzania amesema kuwa, kumekuwa na wimbi kubwa la usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi bila kibali. “Hilo ni kosa kubwa kwa sababu litasababisha nchi yetu kupata baa la njaa huko mbele".

Amesema mipaka ya Tarakea, Holili, Mwanga, Horohoro, Siha, Namanga na Sirari imekuwa inapitisha kiasi kikubwa cha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi jambo ambalo ni hatari sana.

No comments

Powered by Blogger.