-->

Header Ads

Paris Saint-Germain inataka kuifanyia ukatili Manchester United kwa kumsajili Fabinho


Paris Saint-Germain inataka kuifanyia ukatili Manchester United kwa kumsajili Fabinho kwani wapo tayari kutoa kiasi wanachotaka Monaco

Imeripotiwa kuwa Manchester United imeshindwa katika jaribio la kumsajili kiungo wa AS Monaco Fabinho.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu Uingereza inamtamani sana mchezaji huyo matata wa Kibrazili kwa muda sasa, na mchezaji huyo amekiri kuwa angefurahi kufanya kazi na Jose Mourinho.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Daily Record, Paris Saint-Germain wapo mstari wa mbele kuiwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na wapo tayari kutoa dau wanalotaka Monaco.

Kadhalika, Fabinho ambaye amekuwa kwenye rada za United kwa muda mrefu, angekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu kutokana na uwezo wake wa kucheza kama beki wa kati na wa kushoto.

Miaka yake mitatu katika Monte Carlo, amefunga jumla ya mabao 19 katika mechi 139 za michuano yote.

No comments

Powered by Blogger.