MSUVA AIPELEKA STARS ROBO FAONALI COSAFA, SASA KUWAVAA AFRIKA KUSINI..
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeweza kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano ya COSAFA, baada ya kuongoza kundi A huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Angola.
Bao la Saimon Msuva ambaye alitokea bench kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu limetosha kuwavusha Stars ambao wametimiza mechi nne bila kufungwa baada ya kupata sare mbili na kushinda mechi moja na kuvuna point 5.
Baada ya kufunzu hatua ya makundi sasa Stars watakuwa na kibarua kizito cha kuwatoa wenyeji wa mashindano hayo, Afrika kusini. Baada ya hatua hiyo Kama Stars watapita hatua hiyo itakuwa mafanikio makubwa kwa kocha wa Stars Sallum Mayanga ambaye mpaka sasa ameiongoza timu hiyo katika mechi sita bila kupoteza mechi yeyote.
mechi nyingine za hatua za robo fainali zipo kama ifuatavyo.
No comments