MANENO YA TUNDU LISSU KUHUSU SERIKALI KUANZISHA BODI YA USAJILI WA MAWAKILI
Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kimeitisha mkutano wa dharura kujadili na kutoa msimamo wao juu ya mapendekezo ya Serikali kuanzisha Bodi ya Usajili wa Mawakili.
Akifungua mkutano huo leo (Ijumaa Juni 30) wenye lengo la kupata maoni ya wanachama, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla.
Amesema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.
"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa," amesema Lissu.
Lissu ambaye pia ni mbunge, amesema huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo anasema linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya.
No comments