MAMIA WAANDAMANA MAREKANI KUPINGA AMRI YA TRUMP
Nchini Marekani yamefanyika maandamano yaliwahusisha wananchi wa Marekani wanaopinga utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo inayowapiga marufuku raia wa nchi sita zenye idadi kubwa ya Waislamu kuingia Marekani.
Waandamanaji hao waliandamana siku ya jana katika mitaa ya New York na Los Angeles huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga mpango huo.
Hatahivyo mawakili na wanaharakati wa kutetea haki za wahajiri jana walikwenda katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy mjini New York ili kutoa msaada wa kisheria kwa mtu yoyote ambaye anatatizwa na amri hiyo ya Trump.
Waandamanaji hao katika miji ya New York na Los Angeles walisema kuwa amri hiyo ya raisi Trump ni ya kibaguzi, na kwamba haiwezi kuongeza usalama wa Marekani.
Wamesema hatua ya Donald Trump ya kuwapiga marufuku Waislamu wa nchi sita kuingia Marekani ni kitendo cha kibaguzi, chenye kuzusha chuki na kilicho kinyume na thamani za nchi hiyo.
Hatahivo sehemu ya amri hiyo ya Trump ilianza kutekelezwa jana Alhamisi kufuatia mwafaka wa Mahakama Kuu ya Marekani.
No comments