Maneno ya Diddy kwa Jay z na Beyonce juu ya mapacha wao.
Katika usiku wa uzinduzi wa Makala yake inayoitwa"Cant stop, wont stop" ambayo aliizindua usiku wa tarehe 28 mwezi wa 7 rapa Diddy aliamua kutoa ushauri kwa Jay z na Beyonce ambao hivi karibuni wamefanikiwa kupata mapacha.
Diddy ambaye nae ni mzazi wa mapacha wawili wa kike wenye umri wa miaka 10 alisema alipo pata mapacha hao Jay z ndiye alimshauri na sasa ni lazima na yeye amshauri
Diddy alimshauri Jay z na Beyonce kwa kusema kuwa "Jay z and Beyonce should be prepared to double the love,because they are used to getting love from one child.But when get love from two incredible twins its a blessing" akiwa na maana Jay z na Beyonce wajiandae kuongeza mapenzi mara mbili kwa sababu walizoea kupata mapenzi kwa mtoto mmoja,na unapo pata mapenzi kutoka kwa mapacha wawili ni jambo la baraka.
Diddy alisema suala la Jay z na Beyonce kupata mapacha limekuwa ni furaha kwa familia ,marafiki na mashabiki wa wana ndoa hao.
No comments