DIAMOND PLATNUMZ AZINDUA "DIAMOND KARANGA"

Uzinduzi huo umefanika hii leo katika soko la karume jijini Dar es salaam umehudhutiwa na mamia ya wapenzi wa Diamond na Wasafi Classic.
Diamond amesema watanzania wanazidiwa akili na wazungu ambao wanachukua bidhaa zao na kuzipeleka viwandani huku wakiwauzia kwa bei ya juu.
Mkali huyo anayetemba kwa sasa na wimbo wa #i miss you pamoja na #fire aliomshitikisha tiwadavage kutoka Nigeriaamesema ni vyema watanzani kusapot vya kwao ili kukuza uvhumi wa ndani.
Diamond ameongeza kuwa kwa kuwa karanga zake zinaajiri na pia kutengenezwa hapa nchini, ni vyema wadau pamoja na wananchi wote kununua bidhaa hiyo itakayopatikana kwa shilingi 300 tu kwa pakiti moja.
Diamond amekuwa miongoni mwa wasanii wa muziki Afrika wenye mafanikio makubwa ambapo pia namiliki bidhaa nyingine aina ya pafume aliyoizindua hivi karibunina kuiuza kwa shilingi laki moja za kitanzania.
Lebel yake ya WCB imeendelea kuweka gumzo Afrika na duniani baada ya wiki hii msanii chini ya kebel hiyo RAYVANNY kunyakua tuzo ya kimatif y BET katika kipengele cha Intenational best choice viewers award nchini Marekani.
No comments