HII NDIO SABABU YA KENYA KUZUIA WAFANYABIASHARA WA GESI KUTOKA TANZANIA
Serikali imelalamika kuhusu hatua ya Kenya kukataa kuruhusu wafanyibiashara wa Tanzania kuuza gesi ya kupikia nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na katibu wa kudumu katika wizara ya biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda, serikali imegundua kupitia vyombo vya habari mjini Nairobi kwamba Kenya imepiga marufuku uingizaji wa gesi ya kupika kutoka Tanzania kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.
Profesa Mkenda alisema hatua hiyo ya Kenya ni kinyume na makubaliano ya jamii ya Afrika mashariki na makubaliano yalioafikiwa na mataifa hayo mawili baada ya taifa hilo kuiwekea marufuku Tanzania mnamo mwezi Mei 18, 2017.
Kulingana na Profesa Mkenda, hatua hiyo ya Kenya itaathiri wafanyibiashara wakubwa wa kibinafsi na raia wa kawaida ambao hujipatia kipato kupitia biashara ya kuuza gesi .
Kulingana na gazeti la The Citizen hapa nchini, Siku ya Jumatatu katibu maalum nchini Kenya Andrew Kamau alisema kuwa wafanyibiashara hawataruhusiwa kununua gesi kupitia mipakani katika kipindi cha juma moja.
Hatua hiyo kulingana na Kamau ililenga kuzuia kampuni haramu zinazouza gesi ambazo zimeathiri usalama wa taifa hilo.
Katibu huyo aliandikia barua shirika linalodhibiti kawi na shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa KBS na kusema kuwa gesi yoyote ya kupikia inayoingia nchini ni sharti ipitie Mombasa ili kubaini ni wafanyibiashara gani ambao hawana kibali cha kuendesha biashara hiyo.
No comments