TUNISIA: SERIKALI YATANGAZA MAENEO YENYE MAFUTA KUWA YA KIJESHI
Baraza la Usalama wa Taifa la Tunisia limeyatangaza maeneo yanayozalisha mafuta na maliasili nchini humo kuwa ni maeneo ya kijeshi.
Tangazo hilo la kuyaarifisha maeneo hayo kuwa ni ya kijeshi lilipitishwa katika kikao kilichoongozwa na Rais Beji Caid al Sebsi wa Tunisia kilichochunguza hali ya usalama na ya ndani ya nchi; na kutupia jicho pia hali ya kieneo ya taifa hilo.
Rais Beji Caid al Sebsi wa Tunisia Kikao hicho kilichoongozwa na Rais wa Tunisia kimetilia mkazo suala la kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na nchi zinazoendesha mapambano dhidi ya ugaidi ili kutokomeza na kuzuia kupenya ugaidi katika eneo.
Kabla ya kikao hicho, Wizara ya Ulinzi ya Tunisia ilitahadhrisha kuhusu maafa yatakayosabishwa na shambulio lolote katika vituo na taasisi za mafuta za nchi hiyo kufuatia shambulio lililotekelezwa na wapinzani wa serikali.
Wizara hiyo imesisitiza kuwa hali ya usalama na utulivu inashuhudiwa katika taasisi za mafuta za nchi hiyo kufuatia kuwepo vikosi vya jeshi na askari usalama.
No comments