-->

Header Ads

YANGA YAFANYA KUFURU YA USAJILI KWA NGOMA, WATOA KIASI HIKI CHA FEDHA KUNASA SAINI YAKE.

Baada ya kurupushani na tetesi nyingi za usajili juu ya mshambuliaji wa Yanga, Donard Ngoma hatimaye jana amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu yake ya Yanga.
Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili ambao una thamani ya dola 420,00 sawa sawa na milioni 90 za kitanzania. Ngoma amelipwa kiasi hicho "cash" na hivyo hana deni tena na klabu hiyo.

Kiasi alichopokea Ngoma ni mara mbili ya kiasi alichopokea awali wakati anasaini Yanga. Hata hivyo mshahara wa Ngoma bado hujawekwa wazi kuwa atakuwa anaingiza kiasi gani cha fedha kwa mwezi.

kwa kiasi hicho cha fedha ambacho Yanga wametoa "cash' kina maanisha kuwa Yanga sasa wapo sawa kiuchumi ambao ulisemekana uliyumba kidogo. Ikumbukwe Yanga walishindwa kutoa kiasi cha dola 60,000 sawa sawa na milioni 150 kunasa saini ya aliyekuwa nahodha wao Haruna Niyonzima ambaye inasemekana amesaini kwa watani wao wa msimbazi, Simba.

No comments

Powered by Blogger.