-->

Header Ads

FAHAMU KISA CHA MAUAJI YA ASKARI WAWILI PERU

Huko nchini Peru Askari polisi wawili wamepigwa risasi na kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wauzaji wa dawa za kulevya.

Askari hao walishambuliwa walipokuwa wakitoka katika doria kwenye mji wa Apurimac-Ene, mji ambao ni maarufu kwa ukuuzaji wa dawa za kulevya.

Rais wa nchi hiyo Pedro Pablo Kuczynski amesema kuwa wamefanya tukio hilo ikiwa ni kulipiza kisasi cha kuharibiwa kwa zaidi ya kilo 700 za dawa za kulevya.

Biashara ya dawa za kulevya katika jimbo hilo inaendeshwa na kundi la waasi la Shining Path.

No comments

Powered by Blogger.