ASLAY ATOBOA SIRI KUGAWANYIKA YAMOTO

KUFUATIA HOFU YA MASHABIKI WENGI WA KUNDI LA YAMOTO TANZANIA KUDAI KUWA HUENDA KUNDI HILO LIMEVUNJIKA KUTOKANA NA KUGAWANYIKA KATIKA KUFANYA KAZI, MSAA ASLAY ANAYEUNDA KUNDI HILO AMETOA SABABU ZA KILA MMOJA KUFANYA KAZI YAKE BINAFSI NJE YA KUNDI..
Aslay alifunguka hayo na kusema kuwa wao wameamua kuwa kama walivyo wasanii wa kundi la Weusi ambapo msanii anaruhusiwa kufanya ngoma zake mwenyewe na huku bendi nayo ikiendelea kuwa na ngoma zake.
"Mkubwa Fella alitoa tamko akasema sasa hivi ni ruksa kila msanii kutoa nyimbo zake mwenyewe ukiachana na bendi, ila bendi itaendelea kuwepo, ni kama wanavyofanya Weusi msanii mmoja mmoja anafanya kazi zake na kwenye bendi pia yupo" - Aslay.
Msanii huyo ameachia video zake tatu mfululizo "Angekuona", "Usiitie Doa" na "Muhudumu" ambazo zote zinafanya vizuri.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments