ALEXIS SANCHES ANATUA MAN CITY NA SIO BAYERN,
Alexis Sanchez anakaribia kujiunga na Manchester City, kwa mujibu wa habari kutoka Chile
Mshambuliaji huyo wa Arsenal anakaribia kuingia miezi 12 ya mwisho kwenye mkataba wake na amekataa ofa zote za kuongeza mkataba kutoka kwenye klabu hiyo.
Arsene Wenger amezungumzia dhamira yake kumbakisha Sanchez klabuni, akida kuwa ni bora ampoteze bila kupata chochote 2018 kuliko kupokea fedha yoyote tasilimu majira ya joto.
Sanchez Guardiola Manchester City
Lakini, kwa mujibu wa habari kutoka nyumbani kwao Sanchez, Washika Mtutu kwa kusita wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa Man City.
Bayern Munich walikuwa wakimfukuzia kwa bidii nyingi Sanchez wiki za hivi karibuni, lakini mchezaji huyo anataka kubaki Ligi Kuu Uingereza.
Sanchez, ambaye amefunga mabao 30 Arsenal msimu huu, anaweza kuwa usajili wa tatu wa Pep Guardiola majira ya joto ikiwa makubaliano yatafikiwa kutua Etihad.
Kiungo mchezeshaji Bernardo Silva na mlinda mlango Ederson wameshatua City tayari.
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments