-->

Header Ads

WATU WALIOSAHIHI WANAPATIKANAJE?

WATU WALIOSAHIHI WANAPATIKANAJE?


Najua unaweza ukawa na swali kama hili, kutaka kujua nitawezaje kupata mume sahihi au mke sahihi katika maisha yangu?


Jibu ni kwamba Mume au Mke aliye sahihi katika maisha yako “anatengenezwa na wewe mwenyewe na hili siyo kazi ya Mwanaume kama baadhi ya watu wanavyofundisha bali ni kazi ya watu wawili wanaopendana Mwanamke na Mwanaume. Mtu sahihi anaandaliwa mapema maana hata waswahili wanasema “Samaki mkunje angali mbichi” unajua hakuna timu nzuri kama haina wakufunzi wazuri. HIVYO:



a) Mapenzi yanalelewa.
b) Mapenzi yanatafutwa bila kuchoka.
c) Mapenzi yanaandaliwa.
d) Mapenzi yanapaliliwa (Kama shamba).
e) Mapenzi yanatunzwa.
f) Mapenzi ni shule kila siku.
g) Mapenzi Yana mfano wa yai, yanashikwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana, hayachuliwi na mtu mwenye akili za kitoto.
h) Lazima ujue uthamani wake na umuhimu wake katika maisha ya mwanadamu.
i) Mapenzi ni maisha yetu ya kila siku tuliyonayo.
j) Mapenzi yanaishi ndani mtu aliyekubali kujifunza.
k) Mapenzi ni matamu sana ukiyapatia
l) Mapenzi ni machungu sana ukiyakosea.
m) Mapenzi yanakaa kwa mtu anayetamani mabadiliko katika maisha yake.
n) Mapenzi ni uzima katika moyo wa mtu akiyapatia.
o) Mapenzi ni mauti na majuto ukiyakosea.
p) Mapenzi yanaharibu heshima katika jamii ukiyakosea.
q) Mapenzi yanaleta heshima katika jamii ukiyapatia
r) Mapenzi ni kitabu kinachosomwa na kila mtu mdogo na mkubwa.
s) Mapenzi ni bustani nzuri sana inayotengenezwa na mtu, analima, anapanda, anamwagilia maji na kuipalilia.
t) Mapenzi ni maneno matamu yanayoweza kutekenya moyo wa mtu yasiyoweza kumboa mwenzi wako, yakumfanya afurahi, akijisikia kuheshimika, kutambulika, kukubalika, kuthaminika na kupendwa.
u) Mapenzi hayana kiongozi bali katika mapenzi tunaongozana sisi kwa sisi..
v) Katika mapenzi kila mtu anatakiwa kuwa kioo cha mwenzi wake, mrekebishe, mtengeneze, mfanye akubalike katika jamii iliyokuzunguka.
w) Matengenezo ya mapenziyanahitaji muda (time) ya kutosha na mwenzi wako ukiwa na muda wa kutosha utaweza kumfahamu mwenzi wako akichukia anakuaje? Anapofurahi anakuaje? Hata kama kuna wengine huficha makucha yao unatakiwa kuto mitihani ili kufanya (teste) maana hakuna masomo yanayoweza kujifunza yakakosa mithani..
x) Mtihani ni kipimo tosha cha kugundua uelewa wa mtu au mwenzi wako kuwa mtafika katika safari hiyo ya mapenzi au usitishe kutoendelea na safari.
y) Mapenzi ni hadithi nzuri sana iliyokuwa na “mkato (,) nukta (.) na kiulizo (?)
z) Mapenzi ni utiifu, unyenyekevu, upole, usikivu, na matendo.

Mpendwa wangu ukiyajua hayo unaweza ukapata Mume au Mke mzuri sana katika maisha yako, mtengeneze mtu mwanzoni kabisa mwa mapenzi yenu kabla mapenzi hayajakomaa na kuota mizizi. Mimi Silvester Paulo niliyakosea mwanzoni niliumizwa sana, yakaharibu mfumo wangu wa maisha yangu. 
Hivyo nimewahi kuumizwa kimapenzi ijapokuwa ni Mtume, Mchungaji, mapenzi hayaangalii VYEO (TITLE) ulichonacho. 

(Mapenzi ni kitendawili kisichoweza kuteguliwa)” Huu ndio msemo wangu” Leo nimekuwa mwandishi wa vitabu na mwalimu baadaya kujifunza kivitendo. 

Mapenzi ni watu wawili tu na watatu ni Mungu msipoweza kusikilizana ninyi hakuna atakayeweza kukusaidia. Mtengeneze mwenzi wako kwa bidii sana kwa kuwa na muda naye wa kutosha, ukimfundisha, kumonya na kumuombea kwa Mungu ili aweze kuwa mtu wa kufaa kimaisha maana kuumizwa kimapenzi ni kuumizwa kimaisha


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.