-->

Header Ads

WACHEZAJI WATANO RUKSA KUONDOKA YANGA MWISHONI MWA MSIMU HUU, YUPO NGOMA, NIYONZIMA.


Uongozi wa klabu ya Yanga umewaambia wachezaji wake wanaotaka kuondoka katika kikosi chake, “Wanaweza kwenda”.

Imethibitika zaidi ya wachezaji watano wa Yanga, mikataba yao inaisha mwishoni mwa msimu na Yanga imesema kama kuna anayetaka kuondoka hata kama ni kujiunga na Simba, “ruksa”.

Wachezaji waliomaliza mkataba ni pamoja na Yondani na Niyonzima. Vile vile Donald Ngoma ambaye ambaye amekuwa anahusishwa na kujiunga na watani wao Simba mwishoni mwa msimu ingawa mwenyew amekanusha taarifa hizo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema wamezungumza na wachezaji na kuwaeleza.

“Sikia, tumezungumza na wachezaji na kuwaeleza. Sisi kwa sasa tutabaki na mtu ambaye anataka kubaki Yanga.

“Kama kuna mchezaji anataka kuondoka, sawa, ruksa. Lakini kama anataka kubaki tutakaa na kujadili tujue tufanye nini kuongeza mkataba,” alisema Mkemi akizungumza katika kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na runinga ya mtandaoni ya Globaltvonline.

No comments

Powered by Blogger.