-->

Header Ads

Tetesi Muhimu za Usajili Barani Ulaya

Antonio Conte na Jose Mourinho wanataka kumsainisha Mcolombia anayekipiga na Los Blancos,James Rodriguez ambaye hakuwa na msimu mzuri Santiago Bernabeu.
Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Rodriguez mwenye miaka 25 kuamua kuhamia Old Trafford kuungana na Kocha wake wa zamani Jose Mourinho huku thamani yake ikitajwa kufikia pauni milioni 50.

United endapo watafikia bei ya Rodriguez, wana nafasi kubwa zaidi kutokana na mchezaji huyo kuwa chini ya wakala Jorge Mendes ambaye pia anamsimamia Mourinho.

Mchezaji mwingine wa Madrid ambaye huenda akajiunga na Mashetani Wekundu kwa ajili ya msimu ujao ni Gareth Bale. Vyanzo mbalimbali vimedai Bale angependelea kuhamia United kuliko kwenda Chelsea ama kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya Tottenham.

Manchester pia iko katika harakati za kumsaini mchezaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezman na Bernardo Silvo kutoka Monaco.

Majirani wa United, Manchester City nao wako katika vita na mabingwa wa ligi kuu Uingereza timu ya Chelsea wote wakihitaji huduma za beki wa kulia wa Tottenham Hotspurs; Kyle Walker anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 40 kwa sasa. Timu zote mbili ziko tayari kumuongezea Walker mshahara hadi kufikia pauni 140,000 kwa wiki; mara mbili ya mshahara anaolipwa Spurs.

City pia wako kwenye vita kali ya kumsinisha golikipa kinda Gianluigi Donnarumma kutoka klabu ya AC Milan. Guardiola huenda akapata mpinzani kwenye harakati zake za kumpata Donnarumma iwapo Manchester United watamuuza David De Gea kwenda Madrid.

Nchini Ufaransa, klabu ya Lyon inaonekana kukubali kumpoteza mshambuliaji wao tegemeo, Alexandre Lacazzette anayewaniwa na klabu kadhaa zikiwamo Atletico Madrid, Arsenal na Liverpool.

Hata hivyo, Atletico ndio wanaoonekana kuongoza mbio za kumnasa Lacazzette mwenye miaka 25 ambaye katika mechi 43 alizocheza msimu huu, amefanikiwa kucheka na nyavu mara 34. Huko Hispania,

Barcelona huenda wakamwachia Rafinha kujiunga na aidha Liverpool au vibibi vizee vya Turin; Juventus iwapo watafikia bei yake ya Euro milioni 20.

Real Betis nayo imeweka la pauni milioni 3.4 dili mezani kwa ajili ya kupata saini ya Mhispani Nolito. JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.