-->

Header Ads

TAHARUKI YAIBUKA KUHUSU WANAFUNZI WALIOKAMATWA NA MISOKOTO 59 YA BANGI KILIMANJARO

Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili  tofauti huku jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wanafunzi wa Shule ya Msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai kwa kukatatwa na bangi misokoto 59.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Hamisi Issah alisema Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 10:30 Kijiji cha Kyengia wilayani Siha mwananmke mmoja Ephrata Masaki(53), alipigwa na shoti ya umeme wakati akianua nguo.

Alisema nguo hizo zilikuwa zimeanikwa kwenye waya uliokuwa umegusana na waya wa umeme nyumbani kwake na kwamba waya huo ulikuwa umechubuka na kusababisha kifo chake.

Alisema Mei 28, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni, Kata ya Soweto mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sadia Kamote(39), mkazi wa Sanya juu, aligundua kufariki kwa mtoto wake wa darasa la kwanza.

Alisema mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Selemani Said(8) ni wa Shule ya Msingi Kilingi alifariki baada ya kuteleza kutoka kwenye jiwe na kusombwa na maji katika mto Karanga katika daraja la Mangia

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.