-->

Header Ads

TAARIFA KUTOKA TMA KUHUSU UPEPO MKALI


Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya ukanda wa pwani.

Taarifa ya TMA iliyotolewa (Jumatatu) saa 10:00 jioni imesema upepo huo unatarajiwa kuendelea hadi LEO.

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka imesema hali hiyo inatokana na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania. TMA imetoa angalizo kwa watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.