-->

Header Ads

SABABU ZA KANYE WEST KUTOWEKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII




Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi.



Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.
Mkewe nyota wa Reality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.


Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.

Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim Kardashian

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim Kardashian

West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.

Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.


JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,

No comments

Powered by Blogger.