-->

Header Ads

Mc PILIPILI AHAHA kupoteza umaarufu baada ya kukutana na Mc huyu hatari


Master of the ceremony 'MC' anayetajwa kuja kwa kasi katika tasnia ya kusherehesha katika kumbi mbalimbali hapa jijini dar es salaam na mikoa jirani, Mc. BINAGI Ambaye pia kutokana na ujuzi wake na makeke wakati akiwa shughulini kuvutia wadau wengi kumefanya watu wengi kumtaja kama kijana ambaye anahatarisha umaarufu wa Mc. Pilipili ambaye kwa sasa ndiye mwenye mji wake.
MC. BINAGI ambaye kwa mara ya kwanza kusikika na kuonekana katika ukumbi mmoja maarufu hapa mjini aliacha GUMZO Kubwa huku wadau wengi wakitoa maoni yao kuhusu kile wanachokiamini kuwa ndani ya miezi michache ijayo Mc. BINAGI atawaweka chini Ma Mc wengine wakubwa akiwemo Mc pilipili na wengine kama MPOKI, BDOZEN. 

Nidhamu na staha aliyonayo imeonesha pia kuwavutia watu wakubwa na mastaa wengi akiwemo Mc. Pilipili ambaye kupitia ukurasa wake wa instagram alikiri kumkubali kijana huyo na kumsihi kuendelea kupiga kazi. 

MC. BINAGI anawashangaza wengi kutokana na maneno yake matamu na bashasha katika uso wake ambao pia unaambatana na unadhifu wake na muonekano wake wa kuvutia machoni mwa watu.
Mambo mengi yametajwa kuwa sababu ya watu wengi kumuhitaji mc. BINAGI katika sherehe zao na shughuli mbalimbali.

No comments

Powered by Blogger.