NJAA YAMNYIMA SUBIRA MBUNGE WA CCM AFUNGUKA MBELE YA POLEPOLE
Mbulu Vijijini, Flatei Massay |
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay amemuomba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kufikisha kilio cha wananchi kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha njaa.
Massay amesema hayo leo baada ya Polepole kufanya ziara ya siku mbili wilayani Mbulu ya kukagua uhai wa chama, kusikiliza kero na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Mbulu.
Amesema hivi sasa wananchi wana wakati mgumu kutokana na bei kubwa ya vyakula wanavyonunua kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivyo Serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.
Amesema wananchi wa eneo hilo ni hodari kwa kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara, ila kutokana na ukame uliotokea msimu uliopita hivi sasa wanakabiliwa na upungufu wa chakula.
“Kwa sababu chama ndiyo kinasimamia Serikali, kilio hiki cha wananchi tunakifikisha kwako ili tatizo lao limalizike, kwani wanataka chakula cha bei nafuu na siyo kile chakula cha bure,” amesema Massay.
CHANZO: MWANANCHI
JIUNGE NASI AKISI TV KILA SIKU KUPATA HABARI ZA UHAKIKA Nini maoni yako? Weka comment yako hapa,
No comments